Machapisho

USISUMBUE AKILI YAKO NA MANENO YA KUAMBIWA KITU FULANI KINALIPA!

​ USISUMBUE AKILI YAKO NA MANENO YA KUAMBIWA KITU FLANI KINALIPA:- ​ ​ MFANO:- ​ Ukipata nafasi ya kufika kule ​ Mbozi, Mbeya ​ ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na ​ kilimo cha kahawa ​, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli. Wakati unarudi, kama ukishuka ​ Mafinga, Njombe ​ na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na ​ biashara ya miti na mbao ​, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee! Pitia maeneo ya ​ Ruaha Mbuyuni, Iringa ​ kutana na wakulima wa ​ nyanya na vitunguu ​ wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa. Ukitoka pale ukaenda mpaka ​ Mang'ula na Ifakara Morogoro, ​ ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye ​ mpunga ​, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, ...

Maskini Na Tajiri Wanatofautiana Kwa Mambo Haya

Kila kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na mingine midogo ya kawaida. Pia hata wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua. Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge wanyonge. Halikadhalika linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu. Kama mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe na matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo ma...

YAJUE HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MAANA.............????

Picha
YAJUE HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO MAANA.............???? Upendo  ni moja ya hitaji muhimu kwa wanadamu, kila mmoja wetu ahahitaji kupenda na kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba. Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvum...

Zijue Sifa 10 zilizotajwa na HESLB kwa wanafunzi wanaoomba mikopo

Picha
Zijue Sifa 10 zilizotajwa na HESLB kwa wanafunzi wanaoomba mikopo Njombe Yetu blog  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetangaza mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 na imeanza kupokea maombi ya mikopo kuanzia tarehe 6 Agosti 2017 hadi tarehe 4 Septemba, 2017. Waombaji wote wa mikopo watarajiwa wanasisitizwa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 pamoja na taratibu nyingine za uombaji mkopo kabla ya kujaza fomu za maombi ya mkopo zinazopatikana kwenye mtandao wa https://olas.heslb.go.tz Kusoma mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 bofya hapa  www.heslb.go.tz Hapo chini ni sifa za msingi za mwombaji wa mkopo;

Kama Huna Mtaji Na Unahitaji Kuwekeza, Fanya Hivi Kwanza…

Picha
Kama Huna Mtaji Na Unahitaji Kuwekeza, Fanya Hivi Kwanza… Unapokuwa na kiasi fulani cha pesa, na unataka pesa hizo ziongozeke, sina shaka kitu pekee ambacho unachotakiwa kufanya ni kuwekeza pesa hizo ili zikuletee matokeo unayoyataka. Kwa kuwekeza pesa hizo itakusaidia kujenga uchumi imara wa kipesa. Halikadhalika, unapokuwa hauna pesa, kitu gani unachotakiwa kufanya? Pia hapa, unatakiwa kuwekeza vizuri katika rasilimali ulizonazo kama  muda wako, kipaji chako, maarifa, uzoefu wako na hata nguvu ulizonazo.    Kama wenye pesa wanavyowekeza, pia kama huna kitu unatakiwa kuwekeza katika rasilimali hizo za msingi ili kujenga msingi mkubwa wa mafanikio yako kesho. Hutakiwi kulia eti huna pesa, wekeza katika vile ulivyonavyo ndani mwako kwanza. Pia unaweza ukajiuliza nitawekeza vipi wakati sina pesa, sikiliza kuwekeza katika maisha yako haimaanishi kila wakati lazima ukawa unapesa, anza kuwekeza na yale mambo ambayo yatakupa faida kesho. Kivipi hili linawekana? ...