Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

Maskini Na Tajiri Wanatofautiana Kwa Mambo Haya

Kila kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na mingine midogo ya kawaida. Pia hata wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua. Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge wanyonge. Halikadhalika linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu. Kama mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe na matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo ma...