USISUMBUE AKILI YAKO NA MANENO YA KUAMBIWA KITU FULANI KINALIPA!
USISUMBUE AKILI YAKO NA MANENO YA KUAMBIWA KITU FLANI KINALIPA:- MFANO:- Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi, Mbeya ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa , kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli. Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao , unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee! Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa. Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang'ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga , kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, ...